Dkt. Nchimbi: Utafiti Maeneo ya Madini Utaongezeka kwa 50%
Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesisitiza kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, endapo itapewa ridhaa ya kuingia madarakani tena, itahakikisha inatenga maeneo ya kutosha kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini na kuongeza kiwango cha utafiti wa madini kutoka asilimia 16 hadi 50.
Soma Zaidi
DKT.ASANTENI SANA NJOMBE, NIMESHUHUDIA UPENDO NA MAPOKEZI MAKUBWA
Maelfu ya wananchi wa Njombe wamejitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani humo.
Soma Zaidi
KIJANI ILANI CHATBOT – NJOMBE
Wananchi wa Njombe wamechat na *Kijani Ilani ChatBot,* wakijionea moja kwa moja utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020–2025 na kujionea mipango bora ya Ilani ya 2025-2030 katika mkoa wao. Kilimo, Barabara, afya, elimu,Viwanda,Uwekezaji nishati, Huduma bora za jamii maendeleo yanaonekana na kuguswa na wananchi wote.
Soma Zaidi
Rais Samia: Njombe Mmeshuhudia Maendeleo Makubwa, Tutaendelea zaidi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameushukuru mkoa wa Njombe kwa mapokezi makubwa na upendo waliomuonesha alipowasili kwa ajili ya mkutano wa kampeni za CCM. Mapokezi hayo, yaliyojaa shangwe na furaha, yameonesha mshikamano mkubwa wa wananchi na imani yao kwa CCM na viongozi wake.
Soma Zaidi
BALOZI NCHIMBI AHUTUBIA WANANCHI ISAKA, SHINYANGA
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo amehutubia wananchi wa Isaka mkoani Shinyanga baada ya wananchi kumzuilia kwa shangwe kubwa akiwa njiani kuelekea Kagongwa kwa ajili ya Mkutano wa hadhara.
Soma Zaidi
UVCCM HAKUNA KUPOA, TUTAFIKA KILA KONA NA WAGOMBEA WETU
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara, Ndg. Mussa Mwakitinya akiwa ameambatana na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro, Ndg. Ivan Moshi na Mkuu wa Idara ya Uhusiano Kimataifa, Vyuo na Vyuo Vikuu, Ndg. Emanuel Martine wameendelea kumuunga mkono Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiendelea na kampeni mkoani Shinyanga
Soma Zaidi