HONGERENI SANA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2025
14 Oct, 2025
11 Machapisho
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Mohammed Ali Kawaida(MCC) unatoa hongera na pongezi kwa Vijana wenzetu Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 kwa kazi kubwa ya kizalendo, ushujaa, uadilifu na kujitoa kwa moyo mmoja kulitumikia taifa letu.
Tunawapongeza Ndugu Ahmada Hamisi Ahmada, Ndugu Zainabu Suleiman Mbwana, Ndugu Azizi Juma Aboubakar, Ndugu Elizabeth Petro Makingi na Ndugu Comrade Ismail Ali Ussi ambaye ndiye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025. Hongereni sana kwa kuhitimisha kwa mafanikio makubwa mbio za mwaka huu zilizofanyika Mkoani Mbeya, tarehe 14 Oktoba 2025, baada ya safari ndefu na yenye mafanikio mliyoianza Kibaha, Mkoa wa Pwani, tarehe 02 Aprili 2025.
Kwa siku 195 sawa na miezi sita na nusu mmezunguka mikoa yote 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkihamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, mkisisitiza amani, umoja, upendo na mshikamano kama msingi wa taifa lenye ustawi. Mmekuwa vijana bora wa mfano kwetu, uongozi bora, nidhamu na moyo wa kizalendo kwa taifa letu.
Tukikumbuka historia, Mwenge wa Uhuru ni alama ya matumaini iliyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa nia ya: “Kuletea matumaini pale pasipo na matumaini, upendo pale penye chuki na heshima pale palipojaa dharau.”
Kwa namna ya kipekee, UVCCM tunampongeza Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Comrade Ismail Ali Ussi, kwa uongozi wake makini, nidhamu na uthubutu uliowezesha timu kufanikisha mbio hizi kwa mafanikio makubwa na kuendeleza heshima ya taifa letu na heshima ya sisi vijana.
Hongereni sana wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 mmeandika historia ya ushujaa, uzalendo na umoja wa Watanzania.
Kauli mbiu:“Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu.”
#KazinaUtuTunasongaMbele
#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.