UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

DKT. SAMIA AKIZUNGUMZA NA WAPIGA KURA WAKE BUKOMBE

12 Oct, 2025 13 Machapisho
🗓️ Tarehe 12/10/2025
📍Bukombe-Geita

Akiwa katika Uwanja wa Bukombe mkoani Geita, Dkt. Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewasisimua Maelfu ya wananchi waliofurika kumsikiliza kwa shauku na Matumaini makubwa. 

Katika hotuba yake yenye msukumo wa maendeleo amesisitiza kuwa serikali anayoiongoza itaendelea kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya miundombinu, elimu, afya na upatikanaji wa maji safi vijijini na mijini, huku akiahidi kulinda amani, umoja na heshima ya taifa. Dkt. Samia ametoa wito kwa wananchi wa Bukombe na Watanzania wote kwa ujumla kutoka kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025 na kutiki CCM kama ishara ya kuunga mkono kasi ya maendeleo na uongozi wa hekima unaoweka msingi wa Tanzania yenye fursa, utulivu na mafanikio endelevu.

#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki