UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

VIWANDA VYA KUCHAKATA MAZIWA YA NG'OMBE KUJENGWA BUKOMBE

12 Oct, 2025 12 Machapisho
🗓️ Tarehe 12/10/2025
📍 Bukombe -Geita

Katika hotuba yake yenye hamasa kubwa iliyowasha matumaini mapya kwa wananchi wa Bukombe mkoani Geita Dkt. Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametangaza mpango kabambe wa kujenga viwanda vya kisasa vya kuchakata maziwa ya ng’ombe vitakavyobadili Taswira ya uchumi wa mifugo nchini. 

Ameeleza kuwa miradi hiyo itazalisha maelfu ya ajira, kuimarisha soko la maziwa na bidhaa zake na kuongeza kipato cha wafugaji kupitia Uchakataji wa Kisasa, hatua hii Inaashiria Mwelekeo Thabiti wa Dkt. Samia wa kuijenga Bukombe kuwa kitovu cha uzalishaji na uchumi wa Mifugo, Ikidhihirisha dhamira yake ya dhati ya kuinua maisha ya wananchi kupitia Tanzania ya Viwanda na Maendeleo Endelevu.

#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki