MWINYI AKUTANA NA FIRST TIME VOTERS NANGWA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Taifa Ndugu Halid Mwinyi amekutana na kuzungumza na Vijana ambao wanatarajia kupiga kura kwa mara ya kwanza (First Time Voters) wa Chuo cha Ufundi cha Nangwa leo tarehe 22 Septemba, 2025 Wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara.
Soma Zaidi
MBINGA, SERIKALI YA CCM YAAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI
Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itaendelea kuwatumikia wananchi wa Mbinga kwa kuhakikisha inasogeza karibu huduma muhimu za kijamii na kiuchumi, ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara vijijini na mijini, kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya kutolea huduma, pamoja na kuongeza fursa za elimu kwa watoto wa familia zote. Alisema Dkt Samia Suluhu Hassan
Soma Zaidi
ZIARA YA KAMPENI, RUVUMA
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo ataendelea na kampeni zake kuinadi ilani ya CCM Mkoani Ruvuma.
Soma Zaidi
SERIKALI KUENDELEA KUWASHUSHIA NEEMA WAKULIMA WA MBINGA
Mgomba wa kiti cha Urais kupitia tiketi ya CCM DKT SAMIA SULUHU HASSAN ameianza ziara yake ya kampeni mkoani Ruvuma ambapo amebisha hodi akiwa wilayani Mbinga
Soma Zaidi
MBINGA TUMEKUBALIANA CHAGUO LETU DKT. SAMIA
Wananchi wa Mbinga wanafuraha na utayari leo tarehe 21 Septemba 2025 wakipata ugeni wa Mgombea wa Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan akifanya mkutano mdogo kwa kuisemea Ilani ya CCM 2025-2030 na kuomba kura licha ya Wananchi hao kueleza kuwa Chaguo lao ni Dkt. Samia na wagombea wa CCM.
Soma Zaidi
CHEI CHEI CHAKE CHAKE
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan atawasha moto wa Ilani Mkoani Kusini Pemba ambapo atafanya Mkutano Mkubwa wa Hadhara Chake Chake, Gombani Kale leo Ijumaa 19 Septemba, 2025. Vijana wapo tayari kwa nguvu zote kusikiliza Ilani Bora ya CCM 2025-2030 inayogusa maisha ya Kijana na Maisha ya Kila Mtanzania na Sera makini za Maendeleo endelevu ya Taifa letu.
Soma Zaidi