UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Chagueni Viongozi wanaojali amani na maendeleo endelevu ya taifa letu

18 Oct, 2025 10 Machapisho
Zanzibar, 17 Oktoba 2025

Uongozi wa Seneti wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Magharibi, ukiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Ikram Soraga, umeshiriki mafunzo ya elimu kwa mpiga kura katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume (KIST), yakilenga kuwaandaa wanavyuo kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025.

Mafunzo hayo yametolewa na maafisa kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ambapo Mgeni Rasmi, Ndg. Zeyana A. Hamid (Mbunge Mteule wa CCM Viti Maalum UWT – Kundi la Wasomi), amewasihi wanavyuo kudumisha amani, kuendelea kuchagua viongozi wanaohubiri maendeleo, na kuenzi mafanikio makubwa yaliyotekelezwa na Serikali ya CCM hususan katika sekta ya elimu, pamoja na mipango iliyoainishwa kwenye Ilani ya CCM 2025–2030.

Kwa upande wake, Ndg. Ikram Soraga aliwahimiza wanavyuo kuendelea kuwa na imani na Chama Cha Mapinduzi, kujitokeza kwa wingi kupiga kura, na kutokubali kushawishiwa na propaganda zinazolenga kuvuruga amani na umoja wa taifa.

#TokaNitokeTukatiki ✅
#KazinaUtuTunasongaMbele ✅
#ZanzibarMpya ✅