DKT SAMIA AWAPONGEZA VIJANA WA HAMASA
Mgombea wa kiti cha Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akihitimisha Ziara yake Mkoani Kagera amefanya mkutano wa hadhara katika jimbo la Bukoba Mjini na kuwashukuru viongozi wa chama, wananchi vijana wa hamasa na makundi yote kwa ujumla kwa mapokezi na ushiriki wao mzuri wa mikutano yake ndani ya mkoa huo.
Soma Zaidi
DKT.MWINYI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA BIASHARA ENEO LA DARAJANI
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema lengo la Serikali ni kuendelea kuliimarisha eneo la Darajani na kujenga miundombinu zaidi ili wafanyabiashara wapate maeneo mazuri na ya kisasa ya kufanyia biashara.
Soma Zaidi
SERIKALI KUTOA NYENZO NA MITAJI KUWEZESHA UVUVI WA KISASA
Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mgombea wa kiti cha urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi akiwa Wilaya Ya Bukoba Mkoani Kagera amesema kuwa wataimarisha Sekta ya Uvuvi kwa kwa kutoa Nyenzo mbalimbali zitakazosaidia kwenye uvuvi na kutoa mitaji kwa wavuvi.
Soma Zaidi
SERIKALI KUKAMILISHA TAWI LA CHUO KIKUU CHA UDSM KAGERA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Ndugu Samia Suluhu Hassan akiwa Bukoba Mjini, Mkoa wa Kagera, amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika elimu ya juu kwa kukamilisha tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kagera hatua itakayokuza fursa za elimu, kuongeza utafiti na kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Ukanda wa ziwa.
Soma Zaidi
SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA KAGERA
Akiwa Bukoba Mjini Mkoa wa Kagera, Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameonesha dhamira thabiti ya kuendeleza uboreshaji wa miundombinu ya barabara ili kufungua fursa zaidi za kiuchumi, kurahisisha usafirishaji wa mazao na huduma, pamoja na kuunganisha vijiji na miji kupitia barabara za kisasa.
Soma Zaidi
MKUU WA MKOA WA SONGWE AFURAHISHWA NA UBUNIFU WA UVCCM KUPITIA MFUMO WA “KIJANI ILANI CHATBOT
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Jabiri Omari Makame, ametembelea banda la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) katika Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyotamatika katika Viwanja vya Uhindini Jijini Mbeya leo tarehe 14 Oktoba 2025 na kutoa pongezi kwa ubunifu wa kidijitali uliofanywa na vUVCCM chini ya uongozi bora wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Mohamed Ali Kawaida (MCC).
Soma Zaidi