UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

UVCCM Ngome waadhimisha Kuzaliwa CCM kwa Vitendo, wasafisha Soko la Ngome Iringa

31 Jan, 2026 11 Machapisho
Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Tawi la Ngome, Kata ya Kihesa, Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa, wamefanya shughuli ya usafi wa mazingira katika Soko la Ngome kama sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Shughuli hiyo ilihusisha ukusanyaji wa taka, usafi wa maeneo ya biashara na kupanga mazingira ya soko, ikiwa ni ishara ya vitendo ya kuenzi misingi ya CCM ya kujali jamii, kulinda mazingira na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya wananchi.

Vijana wa UVCCM Tawi la Ngome wamesisitiza kuwa wataendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na kijamii, wakizingatia kaulimbiu yao isemayo:
“TUMECHAGUA UMOJA NA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU