UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Mhe. Muhsin Ussi Ashiriki Ugawaji wa Vifaa vya Usafi Zahanati ya Kitunda Kuelekea Miaka 49 ya CCM

02 Feb, 2026 5 Machapisho
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (kundi la Vijana) na Mbunge wa Jimbo la Malindi, Mheshimiwa Muhsin Ussi, ameshiriki katika zoezi la kugawa vifaa vya usafi katika Zahanati ya Kitunda, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Zoezi hilo limeandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ilala, kama sehemu ya shughuli za kijamii zinazoakisi dhamira ya chama katika kuwatumikia wananchi na kuimarisha ustawi wa jamii.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Nasra Mohamed, pamoja na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Hussein Egobano.