UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

VIJANA SHINYANGA WAFUNIKA, WAMUAPISHA DKT. SAMIA KWA KISHINDO CHA OKTOBA TUNATIKI

11 Oct, 2025 15 Machapisho
🗓️ Tarehe 11/10/2025
📍kahama-Shinyanga

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC), ameongoza maelfu ya vijana wa Shinyanga Mjini katika matembezi ya kishindo yaliyojaa hamasa, uzalendo na mshikamano chini ya kaulimbiu ya Oktoba Tunatiki Vijana hao wameonesha umoja wa nguvu ya kizazi kipya, wakiahidi kulinda amani, kudumisha utulivu wa Taifa na kujitoa kwa dhati kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 29 Oktoba 2025, wakisema ndiye kiongozi anayewaletea matumaini, Maendeleo,na Tanzania yenye usawa kwa wote.

Katika tukio hilo lililogeuka kuwa sherehe ya umoja na matumaini ya vijana, sauti za “Tunatiki!” zilitawala mitaa yote ya Shinyanga, zikibeba ujumbe wa imani kwa uongozi wa Dkt. Samia na ahadi ya kuendeleza juhudi zake za kujenga Tanzania yenye fursa, ajira na ustawi wa vijana Shinyanga imetoa Taswira ya Taifa lililo tayari kwa uchaguzi wa amani, huku vijana wakiahidi kuendelea kuwa nguzo imara ya ushindi wa CCM na uendelevu wa maendeleo chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

#OktobaTunatiki✅✅✅
#FyuchaBilaStresi
#TokaNiTokeTukaTiki✅