UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

DKT SAMIA AKIONGEA NA WAPIGA KURA WAKE SHINYANGA MJINI

11 Oct, 2025 12 Machapisho
🗓️ Tarehe 11/10/2025
📍 Shinyanga -Tanzania

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daktari Samia Suluhu Hassan, ameendelea na kampeni zake kwa kishindo akiwa Shinyanga Mjini, ambako amezungumza na Maelfu ya wananchi waliokusanyika kumsikiliza, Akiwa jukwaani Dkt. Samia amesisitiza dhamira ya serikali ya awamu ya sita kuendeleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, maji, afya, elimu na nishati ambayo Imeleta Mapinduzi makubwa katika maisha ya wananchi wa Shinyanga. 

Amehimiza pia umuhimu wa amani, umoja na mshikamano wa kitaifa kama nguzo kuu ya Maendeleo na Ustawi wa Taifa, Daktari Samia amewataka wananchi waendelee kuiamini CCM kwa vitendo vyake, Wakitambua kuwa Chama hicho kimekuwa chachu ya Maendeleo halisi yanayoonekana kote nchini, huku akiwahimiza wapiga kura wote kutoka, kutikisa na kutiki CCM Tarehe 29 Oktoba 2025 ili Kuendeleza Safari ya Maendeleo Isiyoacha mtu Nyuma.

#OktobaTunatiki ✅ ✅ ✅
#Fyuchabilastress
#TokaNitokeTukatiki ✅