UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SERIKALI YA CCM KUTOA HUDUMA YA PEMBEJEO NA BEI ZA PAMBA BURE.

09 Oct, 2025 10 Machapisho
🗓️ Jumatano tar,08/10/2025
📍Mwanza-Tanzamia

Leo akiwa Jijini Mwanza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Samia Suluhu Hassan Ametangaza kwa msisitizo kuwa Serikali ya CCM Itaendelea kutoa huduma ya pembejeo na mbegu za pamba bure kwa wakulima Ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuinua sekta ya kilimo na kuongeza kipato cha wananchi. 

Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha uchumi wa vijijini, kuongeza thamani ya mazao ya wakulima na kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na juhudi za serikali katika kujenga Taifa lenye ustawi, usawa na Maendeleo Endelevu.

#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi
#TokaTutokeTukatiki