UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

📝VIJANA WAZANZIBAR WAFUNGULIWA MILANGO YA AJIRA ZA KIMATAIFA

19 Sep, 2025 16 Machapisho
⏰Ijumaa Tar,19/09/2025
🔛 Zanzibar-Tanzania

Ilani ya CCM 2025–2030 inaleta matumaini mapya kwa vijana wa Zanzibar kupitia mpango Kabambe wa Ajira Kupitia ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wizara ya Mambo ya Nje, mikakati madhubuti imewekwa kuhakikisha vijana wanapata nafasi za ajira ndani na nje ya nchi.

CCM imejipanga kwa vitendo kwa kuendeleza mikataba ya ajira baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali duniani Hatua hii inalenga kuongeza fursa za ajira zenye Staha, kuimarisha ujuzi wa vijana na kupanua upeo wa kipato kwa familia nyingi za Kitanzania, hasa vijana Wanaohitimu elimu ya juu na mafunzo ya ufundi.

Kwa dira hii, vijana wa Zanzibar hawatabaki nyuma tena Ajira za kimataifa zitakuwa chachu ya maendeleo, zikijenga kizazi chenye matumaini, heshima na uwezo wa kushindana katika Soko la dunia, Ni wakati wa kuamini, kushirikiana na kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Oktoba Tunatiki, Kijani Tumetulia, Fyucha Bila Stresi.
 #KaziNaUtuTunasongaMbele
#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi