SERIKALI ITAJENGA MATENKI MAKUBWA 3 YA KUHIFADHI MAFUTA ZANZIBAR
16 Sep, 2025
36 Machapisho
🗓️ 15 Septemba 2025
📍 Pemba-Zanzibar
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya CCM ambae pia ni rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, Leo amezindua kampeni Gombani-Zanzibar.
Katika uzinduzi huo, Dkt. Mwinyi alisema, kuna wakati nchi yetu mfumuko wa bei unaongezeka kutokana na kupanda kwa mafuta ya petroli na diseli, hivyo serikali itakwenda kujenga matanki makubwa 3 ya kuhifadhi mafuta angalau miezi 3 yakae ndani ya Nchi yetu ili tusikose na kuathirika na upandaji wa bei ya mafuta nchini."
Dkt. Mwinyi aliongeza kuwa, hifadhi hii ya mafuta itasaidia kupunguza mfumuko wa bei ya bidhaa katika Nchi yetu.
#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.