UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

JE, UMEUONA MKONO WA MAMA ITIGI-SINGIDA?

09 Sep, 2025 42 Machapisho
Leo ni siku ya kihistoria kwa wananchi wa Itigi, Singida, ambao wamejumuika kwa Shauku kubwa kumpokea Dkt Samia Suluhu Hassan Mgombea wa Urais aliyeonyesha nyuso za furaha, akiwapungia mikono wananchi na wakazi wa Itigi, akionyesha ukaribu na upendo kwa kila mmoja, Sasa ni wakati wa kuungana, kuimarisha mshikamano wa wananchi na kuonyesha upendo kwa Maendeleo.

Katika mkutano huu wa kampeni, wananchi walipata nafasi ya kusikia kwa ukaribu sera na mipango ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya kila Mwana-Itigi,Singida na Taifa Kwa Ujumla, Ukitiki Kwa Mama Umetiki Kwa Maendeleo Bila Stresi,.

Ni hakika kuwa uongozi wa Mama Dkt Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM unalenga kuhakikisha kila sekta ya kijamii na kiuchumi inasonga mbele Kutoa elimu bora, afya kwa wote, kilimo cha kisasa, miundombinu ya barabara na maji hadi uwezeshaji wa vijana na wanawake yote yameelezwa kwa uwazi na shauku, Wananchi wa Itigi wamepata motisha na matumaini mapya ya maisha bora kupitia mpango huu wa maendeleo.

#KaziNaUtuTunasongaMbele
#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi