UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

KARIBU SANA MAMA, MAKAMBAKO TUPO PAMOJA NAWE

06 Sep, 2025 23 Machapisho
Mapema asubuhi ya leo, maelfu ya wananchi wa Makambako wamejitokeza kwa wingi wakiwa na furaha, hamasa na shangwe kubwa kumsubiri Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

" Wananchi hawa wamesema wako tayari kumsikiliza Mama akijinadi kwa sera bora za CCM na kueleza ahadi za maendeleo endelevu kwa Watanzania wote."

Makambako wamesimama imara hawana shaka na kwa pamoja  wanasema “Maendeleo wameyaona, hakuna kama Mama, Oktoba watatiki kwa kishindo 🙌 

Zaidi ya hapo, wakazi wa Makambako wamesema leo wanajambo leo na Mama kama ishara ya mapenzi na heshima yao kwake. 🔥 🔥 

#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi 
#KazinaUtuTunasongaMbele 
#TunazimaZoteTunawashaKijani