UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MWINYI: MFUMO WA ILANI KIJANI CHATBOT UNA MAMBO MATATU

25 Aug, 2025 34 Machapisho

Dar es Salaam, 25 Agosti 2025 — Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Ndg. Halid Mwinyi, ameeleza kuwa mfumo mpya wa kisasa wa Ilani Kijani Chatbot utarahisisha kwa kiasi kikubwa utoaji wa elimu kwa vijana wa Kitanzania juu ya fursa na mipango ya maendeleo iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2025–2030).

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam, Mwinyi alisema kuwa chatbot hiyo inakuja na dhamira mahsusi ya kusaidia vijana kuelewa kwa undani utekelezaji wa ilani na nafasi yao katika mchakato wa maendeleo ya taifa.

“Katika kuzindua mfumo huu, tumelenga mambo matatu makuu,” alisema Mwinyi.

Malengo Matatu ya Mfumo wa Ilani Kijani Chatbot:

  1. Kutoa taarifa za haraka, sahihi na za kidijitali kuhusu Ilani ya CCM, miradi ya maendeleo na namna jamii hususani vijana wanavyonufaika.

  2. Kuwezesha vijana kuuliza maswali na kupata majibu ya moja kwa moja kupitia mfumo huu wa kisasa.

  3. Kuongeza uelewa wa vijana kuhusu nafasi zao katika maendeleo ya taifa na ushiriki wa kisiasa, huku ukikuza matumizi ya Artificial Intelligence na majukwaa ya kidijitali katika elimu ya siasa, utawala bora na demokrasia.

Mwinyi aliongeza kuwa chatbot hiyo ni nyenzo muhimu kwa kizazi cha sasa cha kidijitali na itakuwa chachu ya vijana kushiriki kikamilifu katika mabadiliko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.


🔖 KazinaUtuTunasongaMbele
💡 TunazimaZoteTunawashaKijani
OktobatunatikiFyuchaBilaStresi