Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC), amewataka Watanzania kutumia programu bunifu ya Kijani Ilani Chatbot kama nyenzo ya kupata taarifa sahihi kuhusu Ilani ya CCM na utekelezaji wake, ili kuongeza uelewa na kukabiliana na upotoshaji unaoenezwa na watu wasiolitakia mema Taifa.
Akizungumza jana, Agosti 25, wakati wa uzinduzi wa Kijani Ilani Chatbot uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, Ndg. Kawaida alisema kelele zinazopigwa na wapotoshaji hazina mashiko, kwani hoja zao hazina majibu ya msingi.
“Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, mwanachama yeyote anayetaka kushauri viongozi au serikali ana nafasi ya kufanya hivyo, lakini kuna utaratibu wa kufuata. CCM ni taasisi kubwa, siyo sehemu ya waropokaji,” alisema Ndg. Kawaida.
Aidha, alitumia fursa hiyo mbele ya maelfu ya vijana kutoka pembe zote za Tanzania kutoa shukrani za dhati kwa Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake, Ndg. Jokate Urban Mwegelo, kwa mchango mkubwa alioutoa ndani ya UVCCM, na kumtakia kila la heri katika majukumu yake mapya ya kuendeleza chama na kujenga Taifa.
✅ #OktobaTunaTiki
✅ #KazinaUtutuTunasongaMbele
✅ #TunazimazoTunawashaKijani