UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

ZANZIBAR YANG'ARA : CCM GALA DINNER 2025 ZACHANGWA BILIONI 5.93

17 Aug, 2025 28 Machapisho

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza kwa kishindo hafla ya “CCM Gala Dinner 2025” iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip – Zanzibar, mnamo Agosti 17, 2025 kuanzia saa 11 jioni.

Baada ya mafanikio makubwa ya Gala Dinner ya Bara, sasa mwenge wa mshikamano na mshereheko umeendelea Visiwani Zanzibar kwa kishindo kikubwa. Hafla hii maalumu ya harambee imewaleta pamoja viongozi, vijana, wanachama na wadau mbalimbali walioujaza ukumbi kwa mapenzi ya dhati kwa chama chao kipenzi.

Katika tukio hilo la kihistoria, CCM imefanikiwa kuchangisha jumla ya Shilingi Bilioni 5.93, ikidhihirisha imani kubwa na mshikamano wa watanzania kuelekea ushindi wa chama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Mapenzi makubwa kwa viongozi wetu

Wanachama na wananchi walionekana kwa hamsa kubwa, wakimpa heshima na mapenzi ya dhati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakionyesha mshikamano na imani kubwa kwa  Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kukipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa uongozi wake bora. Vijana walijitokeza kwa wingi, wakichangia kwa hamasa kubwa na kuonyesha kuwa ndilo jeshi kubwa la ushindi wa CCM.

Hamasa ya kuchangia inaendelea

Mchango wa Zanzibar umekuwa ni ishara ya nguvu ya chama. Wananchi wanaendelea kuchangia kwa kasi kubwa kila kona ya nchi kuhakikisha chama kinajipanga ipasavyo kuelekea uchaguzi mwezi oktoba 2025.

👉 Jinsi ya Kuchangia kupitia Simu

  1. Piga: *150*50*1#

  2. Ingiza Control Number: C02025

  3. Weka Kiasi cha Mchango

  4. Ingiza PIN yako kuthibitisha

📌 Michango itaendelea kupokelewa hadi Agosti 27, 2025 – kila mchango wako ni nguvu ya ushindi wa CCM na dhamira ya maendeleo kwa kila Mtanzania,Tuendelee kuchangia kwa kasi