UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MAELFU WAJITOKEZA KUMSINDIKIZA DKT.SAMIA KUCHUKUA FOMU

09 Aug, 2025 36 Machapisho

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgombea mwenza wake Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, wamechukua rasmi fomu za kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Tukio hilo limefanyika , Agosti 9, 2025, katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) zilizopo Njedengwa, Dodoma.

Mapokezi ya Kishindo

Maelfu ya wananchi, wanachama na wapenzi wa CCM kutoka kila pembe ya Tanzania Bara na Visiwani walijitokeza kwa wingi kwa mapenzi na imani yao kubwa kwa mgombea wao Dkt. Samia. Viwanja vya Makao Makuu ya CCM – Dodoma vilifurika umati wa watu waliobeba mabango zenye jumbe za kuhamasisha ushindi wa chama, huku wakipaza sauti za kumshangilia Rais Samia na mgombea mwenza wake. Wananchi walikuwa wenye furaha kubwa baada ya kuona Dkt.Samia kachukua fomu

Barabara kuu za Dodoma zilijaa wananchi waliokuwa wakisubiri kwa hamu msafara wa wagombea wetu, wengi wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kishindo kama vile:“Oktoba Tunakiti!”“Samia ni Tumaini la Watanzania”“Dkt Samia Chaguo letu” “Kazi na utu,tunasonga mbele", n.k

Ushuhuda wa mapenzi na imani ya wananchi

Wakati wa tukio hilo, ilidhihirika wazi kuwa watanzania wana imani kubwa na mapenzi ya dhati kwa CCM na mgombea wake Dkt. Samia, ambaye ameendelea kuaminika kutokana na uongozi wake bora wa kidiplomasia na wa maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwashukuru wananchi wote kwa kujitokeza kwa wingi na kusimama bega kwa bega na chama chao. Aliahidi kuendeleza kasi ya maendeleo, mshikamano wa kitaifa na ujenzi wa Taifa lenye matumaini makubwa kwa sasa na baadaye