CCM YAANZA HARAMBEE YA UCHAGUZI: WANANCHI WAIPOKEA KWA MIKONO MIWILI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumezindua rasmi harambee ya kuchangia kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 na kufanikisha kukusanya Shilingi Bilioni 86.31 katika uzinduzi uliofanyika Agosti 12, 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Uzinduzi huu umepokelewa kwa shangwe na wananchi, wafanyabiashara, wadau wa maendeleo na wanachama wa CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Rais Samia Suluhu Hassan. Katika harambee hiyo, Rais Samia alichangia Sh. Milioni 100, huku Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akichangia Sh. Milioni 50.
Jumla ya fedha taslimu zilizokusanywa ni Sh. Bilioni 56.31, huku Sh. Bilioni 30.2 zikiwa ahadi. Hii ni sehemu ya lengo kubwa la chama kukusanya Sh. Bilioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya ushindi wa kishindo wa CCM katika uchaguzi wa 2025.
Akizungumza baada ya kupokelewa kwa michango hiyo, Rais Samia alisema:
“Kutoa ni moyo siyo utajiri. Michango yenu ndiyo ngao ya ushindi wetu na dhamira ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.”
Aidha, aliwahimiza wananchi wote kuendelea kushiriki harambee hii, wakiwemo Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora).
👉 Jinsi ya Kuchangia kupitia Simu:
-
Piga:
*150*50*1# -
Ingiza Control Number:
C02025 -
Weka Kiasi cha Mchango
-
Ingiza PIN yako kuthibitisha
Michango hii itaendelea kupokelewa hadi Agosti 27, 2025. Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amewahimiza Watanzania wote wenye mapenzi mema kuendelea kushiriki, akisisitiza kuwa hatua hii ni muhimu katika kuandaa ushindi wa chama kinachobeba matumaini ya wananchi
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.