UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

TAARIFA KUTOKA KWA MHESHIMIWA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

08 Dec, 2025 14 Machapisho
Katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Uhuru Kesho, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Waziri Mkuu leo, ametoa agizo maalum kwa wananchi wote wa Tanzania.

Mheshimiwa Rais ameelekeza kuwa KILA MTANZANIA ASHIRIKI maadhimisho ya kesho akiwa nyumbani, kama njia ya kutafakari historia ya taifa, kutambua thamani ya uhuru wetu, na kuenzi misingi ya amani na umoja iliyojengwa kwa miaka mingi.

Hata hivyo, agizo hilo halimhusu mfanyakazi ambaye kazi yake ni ya lazima na haiwezi kusimama, wakiwemo madaktari, wauguzi, askari wa ulinzi na usalama, pamoja na watumishi wanaohitajika kwa dharura au huduma muhimu za moja kwa moja kwa wananchi. Watumishi hao wataendelea kutimiza majukumu yao kama kawaida ili kuhakikisha huduma muhimu hazikatiki.

Serikali imesisitiza kuwa maadhimisho haya yawe ya utulivu, uzalendo na umoja, na wananchi wote wanahimizwa kutumia siku hii kutafakari hatua tulizopiga na kujipanga kuendelea kulijenga taifa letu katika misingi ya maendeleo na mshikamano.

#KazinautuTunasongaMbele
#KeshoHatokiMtu