UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

KAWAIDA: VIJANA, TUNAJUKUMU LA KULINDA AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO WA TAIFA LETU

07 Dec, 2025 19 Machapisho

Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Mohammed Ali Kawaida(MCC) amesisitiza wito wa mshikamano na amani miongoni mwa Watanzania, huku akibainisha mafanikio makubwa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dodoma, 07 Desemba 2025 – Katika Kikao Kazi cha Viongozi wa UVCCM ngazi ya Taifa, Mikoa, Wilaya na Seneti kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Kawaida amewaomba vijana na Watanzania wote kutotumika kuharibu amani ya nchi.

 "Niwaombe tena na tena, Vijana na Watanzania wote, tusiendelee kujiumiza wenyewe kwa kushawishiwa na watu ambao hawapo Tanzania. Hatuna nchi nyingine. Nchi yetu ni Tanzania; lazima tuilinde na tuiheshimu," alisema Kawaida.

Kawaida pia amesisitiza mafanikio ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan:

  • Kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi
  • Ujenzi wa vituo vya afya, hospitali za wilaya, na zahanati
  • Kuendeleza elimu kupitia shule na vyuo vya VETA
  • Kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari
  • Kufutwa kwa kesi za kisiasa
Maoni ya Mwandishi: Kwa mtazamo wangu, hotuba ya Kawaida   inasisitiza mshikamano na amani lakink pia inawakumbusha vijana kuwa maendeleo ya taifa hayaji kwa bahati, bali kwa ushirikiano, uwajibikaji, na upendo kwa nchi. Kwa hakika, wito huu ni sahihi katika mazingira ya kisiasa ambapo amani na mshikamano vinaweza kudhuriwa na watu wenye nia mbaya. Hii ni fursa kwa vijana kuonyesha uzalendo wao kwa vitendo, sio maneno tu.

Kikao hiki kinaonesha wazi dhamira UVCCM katika kukuza uzalendo, mshikamano wa kitaifa, na ushirikiano miongoni mwa vijana wote wa Kitanzania.Kawaida amehimiza kuwa kila Mtanzania ana jukumu la kulinda amani na mshikamano wa taifa, jambo linalopaswa kuwa kielelezo cha kila kijana anayependa Tanzania.

#KazinaUtutunasongambele