UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

RAIS SAMIA ATWAA TUZO YA KIMATAIFA YA MAJI

14 Aug, 2025 44 Machapisho


Johannesburg, Afrika Kusini – 14 Agosti 2025:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Maji – Presidential Water Changemakers Award 2025 na Global Water Partnership kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika. Hafla ya tuzo hiyo imefanyika katika Mkutano wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Afrika (AU–AIP Africa Water Investment Summit 2025) unaoendelea jijini Johannesburg kuanzia tarehe 13–15 Agosti 2025.

Tuzo hii imetolewa kwa kutambua mchango wa kipekee wa Rais Dkt. Samia katika kuongoza mageuzi makubwa ya sekta ya maji nchini Tanzania, hatua ambazo zimeboresha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi wa mijini na vijijini.

Chini ya uongozi wake:

  • Upatikanaji wa maji vijijini umeongezeka kufikia 79.6%
  • Upatikanaji wa maji mijini umefikia 90%
  • Miradi mikubwa 1,633 ya usambazaji maji imekamilika
  • Vituo vipya vya maji 107,819 vimejengwa
  • Zaidi ya wananchi milioni 12 wamenufaika moja kwa moja
  • Vijiji 196,160 vimefikiwa na huduma ya maji

Mageuzi haya yameiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kama mfano wa taifa linalowekeza kwa vitendo katika huduma za kijamii, hususan maji safi na salama.