UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SERIKALI KUJENGA STENDI NA SOKO LA KISASA NKASI

18 Oct, 2025 9 Machapisho
🗓️ Jumamosi 18 Oktoba,2025
📍Rukwa-Nkasi

Mgomba Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali yake itajenga stand na soko la kisasa Nkasi ili kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza mapato ya wafanyabiashara. 

Akiongea na wananchi, Dkt. Samia amesema ujenzi wa soko hilo utakuwa na Miundombinu ya kisasa ambayo itawawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa urahisi na kuongeza tija, Aidha amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itaendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo ambayo itawanufaisha moja kwa moja wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

#oktobatunatikiâś…âś…âś…
#fyuchabilastresi 
#tokanitoketukatiki âś…