UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

DKT. SAMIA: TUMEMPOTEZA KIONGOZI MAHIRI NA MPENDA AMANI

15 Oct, 2025 7 Machapisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, akimtaja kuwa kiongozi mahiri, Mwanamajumui wa Afrika, mpenda amani na mtafuta suluhu.

Amesema Raila alikuwa na ushawishi na upendo uliovuka mipaka ya Kenya na kwamba msiba huu sio wa Wakenya pekee, bali pia ni wa Watanzania na Waafrika wote.

“Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa Rais wa Kenya, Mheshimiwa Dkt. William Samoei Ruto, Mama Ida Odinga, watoto, familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Kenya kwa msiba huu,” amesema Rais Dkt.  Samia.

Aidha, Rais Samia ameungana na familia ya Odinga kuwaombea faraja, subra na imani katika kipindi hiki kigumu, huku akiomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mheshimiwa Raila Amolo Odinga mahali pema peponi, Aamiin .

#KazinaUtuTunasongaMbele 
#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi 
#TokaNitokeTukatiki. 
#TunazimaZoteTunawashaKijani