UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Yohana Tegemea Joseph (Joh Music)

Yohana Tegemea Joseph (Joh Music)

Umri: 28 Msakuzi, Kata ya Kwembe, Jimbo la Kibamba, Wilaya ya Ubungo, Mkoa wa Dar es Salaam Dar es Salaam Bachelor of Science in Social Protection kutoka Institute of Finance Management
Yohana Tegemea Joseph anajulikana kama kama Joh Music ni kijana mbunifu, kiongozi na msanii wa muziki wa kizalendo anayehudumu kama Katibu wa UVCCM Tawi la Msakuzi. Amejikita katika uhamasishaji wa vijana kupitia sanaa, uongozi na teknolojia, huku akiwa mwanzilishi wa mradi wa UVCCM Msakuzi TV unaolenga kuhabarisha jamii na kuwa chanzo cha mapato endelevu.

Historia na Wasifu

Yohana Tegemea Joseph ni kijana mwenye maono makubwa katika uongozi na maendeleo ya vijana. Kwa sasa anahudumu kama Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Msakuzi, akisimamia shughuli mbalimbali za jumuiya na kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za kijamii, kisiasa na maendeleo ya vijana. Mbali na nafasi yake ya kiuongozi, Yohana ni msanii anayejulikana kwa jina la Joh Music, ambapo kupitia nyimbo zake za kizalendo amekuwa akihamasisha jamii kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi pamoja na serikali ya Samia Suluhu Hassan. Katika ubunifu wake, ameanzisha mradi wa UVCCM Msakuzi TV, chombo cha habari cha mtandaoni kinachotumika kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii kupitia majukwaa ya kidijitali kama Instagram na YouTube.

Mafanikio

1.Kuanzisha na kuendesha mradi wa UVCCM Msakuzi TV kwa zaidi ya mwaka mmoja.
2.Kuandika na kutoa nyimbo za kizalendo zinazohamasisha vijana na jamii.
3.Kujenga ushawishi wa kidijitali kupitia maudhui ya habari na elimu mtandaoni.
4. Kuongoza shughuli za vijana katika tawi la Msakuzi kwa mafanikio.
5. Kuchangia mawasiliano kati ya viongozi na wananchi kupitia media ya kisasa.

Changamoto Nilizopita

1.Ukosefu wa vifaa vya kisasa vya media kama kamera za kurekodia maudhui bora.
2.Ufinyu wa rasilimali za kifedha katika kuendeleza mradi wa media.
3.Changamoto ya kupata maudhui ya video ya moja kwa moja bila kutegemea vyanzo vya nje.

Ushauri kwa Vijana Wengine

Vijana wanapaswa kutumia vipaji walivyonavyo kama nyenzo ya maendeleo binafsi na ya jamii. Ubunifu, nidhamu, kujifunza kila siku na kutokata tamaa ni msingi muhimu wa mafanikio. Teknolojia ya kisasa inaweza kuwa fursa kubwa ikiwa itatumika kwa malengo sahihi
Rudi kwa Vijana Wenye Mafanikio

Vijana Wengine Wenye Mafanikio

Nafidh Ally Mola
Nafidh Ally Mola

Nafidh Ally Mola ni kijana mbunifu wa teknolojia na akili mnunde (AI) kutoka Tanzania mwenye umri wa miaka 20. Ametambuliwa kitaifa na kimataifa kwa ubunifu wake katika TEHAMA, ikiwa ni pamoja na kushiriki Global Misk Forum na kutunukiwa tuzo ya Best AI Innovator in Africa kupitia AUDA-NEPAD. Ni kijina mbunifu na mwenye mawazo chanya ya kutumia teknolojia katika kutatua changamoto za jamii

Soma Hadithi Yake