Wasifu wa Vijana
Soma safari zao za mafanikio, changamoto walizopita, na ushauri wao
Yohana Tegemea Joseph (Joh Music)
Yohana Tegemea Joseph anajulikana kama kama Joh Music ni kijana mbunifu, kiongozi na msanii wa muziki wa kizalendo anayehudumu kama Katibu wa UVCCM Tawi la Msakuzi. Amejikita katika uhamasishaji wa vijana kupitia sanaa, uongozi na teknolojia, huku akiwa mwanzilishi wa mradi wa UVCCM Msakuzi TV unaolenga kuhabarisha jamii na kuwa chanzo cha mapato endelevu.
Nafidh Ally Mola
Nafidh Ally Mola ni kijana mbunifu wa teknolojia na akili mnunde (AI) kutoka Tanzania mwenye umri wa miaka 20. Ametambuliwa kitaifa na kimataifa kwa ubunifu wake katika TEHAMA, ikiwa ni pamoja na kushiriki Global Misk Forum na kutunukiwa tuzo ya Best AI Innovator in Africa kupitia AUDA-NEPAD. Ni kijina mbunifu na mwenye mawazo chanya ya kutumia teknolojia katika kutatua changamoto za jamii
Unataka Kutajwa hapa?
Umejifunza na kupata mafanikio fulani? Wasiliana nasi na tueleze safari yako