Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Tangazo la Fursa: Udahili wa Nafasi za Masomo Nchini China 2026/2027 | Fursa za Vijana | UVCCM

Tangazo la Fursa: Udahili wa Nafasi za Masomo Nchini China 2026/2027

Udhamini wa Masomo Muhimu Maombi yameisha
3
Wameona
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Chinese Government Scholarship (CGS)
Shirika
Vyuo Vikuu mbalimbali nchini China
Mahali

Maelezo ya Fursa

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China inawatangazia Watanzania wenye sifa kutuma maombi ya ufadhili kamili (Chinese Government Scholarship) kwa ajili ya masomo ya Shahada, Uzamili na Uzamivu kwa mwaka wa masomo 2026/2027. Ufadhili huu unagharamia ada zote, malazi, posho ya kujikimu, bima ya afya, na gharama za msingi za maisha nchini China.
Maombi yanapaswa kuwasilishwa mtandaoni kupitia mfumo wa CGS na nyaraka zote kutumwa kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kabla ya tarehe ya mwisho.

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imetoa ufadhili kamili wa masomo (Chinese Government Scholarship) kwa ajili ya Watanzania wanaotaka kusoma Shahada, Uzamili na Uzamivu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini China kwa mwaka wa masomo 2026/2027.

Huu ni ufadhili unaojumuisha gharama zote muhimu ikiwemo ada ya masomo, malazi, posho ya kujikimu, bima ya afya, pamoja na fursa ya kujifunza lugha ya Kichina kwa baadhi ya programu. Waombaji wenye sifa wanahimizwa kuchukua hatua mapema na kukamilisha maombi mtandaoni kupitia mfumo wa CGS.

Mahitaji ya Kujiunga



Fomu ya maombi ya CGS iliyojaa mtandaoni

Vyeti na transcripts vilivyothibitishwa (CSEE, ACSEE, Diploma, Bachelor, Master)

Mpango wa masomo (Study Plan/Research Proposal)

Barua 2 za mapendekezo (kwa Uzamili & Uzamivu)

Cheti cha HSK / IELTS / TOEFL kutegemea lugha ya masomo

Cheti cha kuzaliwa

Cheti cha kutokuwa na rekodi ya uhalifu

Fomu ya uchunguzi wa afya

Pre-admission letter au admission notice (ikiwa inahitajika)

Masharti ya Kustahiki

Awe raia wa Tanzania

Awe na ufaulu mzuri katika masomo

Umri usiozidi miaka 25 kwa Shahada, 35 kwa Uzamili, na 40 kwa Uzamivu

Awe na pasi ya kusafiria au uthibitisho kuwa ameomba

Awe na afya njema

Awe na vyeti na transcripts vilivyothibitishwa

Faida na Manufaa

Ufadhili kamili wa ada zote za masomo

Malazi ya chuo (hostel)

Posho ya kujikimu (monthly living allowance)

Bima ya afya

Mafunzo ya lugha ya Kichina (kwa baadhi ya programu)

Fursa za kusoma katika vyuo bora vya China

Nafasi ya upanuzi wa upeo, ujuzi na mitandao ya kimataifa