UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

KISHINDO CHA DKT.NCHIMBI NYANG'HWALE NI USHINDI TU

05 Sep, 2025 69 Machapisho
Maelfu ya wananchi wa Nyang’hwale, mkoani Geita leo Septemba 5, 2025 wamejitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Saba Saba kumpokea na kumsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiendelea na mikutano ya kampeni za CCM. Mapokezi hayo yameonesha imani kubwa ya wananchi kwa CCM na kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa CCM.

Akihutubia wananchi, Dkt. Nchimbi amewataka kujiandaa kwa Oktoba 29 kuhakikisha kura zote za kishindo ni za CCM. Amebainisha kuwa chama hicho kimeendelea kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli kupitia miradi ya afya, elimu, kilimo, viwanda na nishati, hivyo wananchi hawana sababu ya kuyumba. Pia aliwanadi wagombea wa ubunge na udiwani akiwemo Hallen Nassor Amar (Buldoza), Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nyang’hwale.

Wananchi wa Nyang’hwale walilipuka kwa shangwe na hamasa kubwa wakiahidi kwa sauti moja kuwa hawatapoteza kura hata moja nje ya CCM.  Nyang’hwale waapa kuwa 29 Oktoba ni ushindi wa kishindo kwa Dkt. Samia na ubunge CCM na kwa  madiwani wa CCM.

#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi 
#KazinaUtuTunasongaMbele 
#TunazimaZoteTunawashaKijani