Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KUWASILI KWA WAJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM UKUMBI WA NEC (WHITE HOUSE), DODOMA | UVCCM
Habari za Kitaifa (UVCCM) Kipaumbele

KUWASILI KWA WAJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM UKUMBI WA NEC (WHITE HOUSE), DODOMA

11 Jul, 2026 Admin User 165 views min read

Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wameanza kuwasili katika Ukumbi wa NEC (White House), Makao Makuu ya CCM, Dodoma, kwa ajili ya Kikao cha Baraza Kuu la UVCCM kinachofanyika leo, tarehe 11 Julai 2026.

Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Mohamed Ali Kawaida (MCC), ambapo Baraza litajadili masuala mbalimbali muhimu yanayohusu maendeleo ya Umoja na utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba na miongozo ya Chama.

#KaziNaUtuTunasongaMbele