Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KAWAIDA: HATUTAWAVUMILIA WATUMISHI WANAOKWAMISHA VIJANA KUPATA MIKOPO | UVCCM
Habari za Kitaifa (UVCCM) Kipaumbele

KAWAIDA: HATUTAWAVUMILIA WATUMISHI WANAOKWAMISHA VIJANA KUPATA MIKOPO

19 May, 2026 Admin User 33 views min read

Na Mwandishi Wetu, Tandahimba – Mtwara

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mohammed Ali Kawaida amesema ataendelea kusimamia maslahi ya vijana nchini kwa kuhakikisha wanapata fursa, huduma na mazingira rafiki yatakayowawezesha kutimiza malengo yao ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza leo na vikundi vya vijana wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 katika Wilaya ya Tandahimba, Ndugu Kawaida alisema hatakuwa tayari kuvumilia watumishi wanaokwamisha upatikanaji wa mikopo kwa vijana, wanawake na makundi maalum wenye sifa za kunufaika na fedha hizo.

Alisema watumishi wa umma wana wajibu wa kuwasaidia vijana kwa uadilifu na weledi, hususan katika kuwawezesha kupata mikopo ya serikali, mafunzo, pamoja na fursa mbalimbali za kiuchumi zinazolenga kuongeza ajira na kipato kwa vijana.

“Tutahakikisha vijana wanapata haki yao. Serikali imeweka mazingira na fedha za kuwawezesha, hivyo hakuna sababu ya baadhi ya watumishi kuwa kikwazo kwa vijana wanaotafuta maendeleo yao,” alisema Kawaida.

Kwa upande wao, vikundi vya vijana vilivyonufaika na mkopo wa pikipiki katika maeneo ya Tandahimba Mjini pamoja na kijiji cha Nachunyu, vimeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza ahadi ya kuwainua vijana kiuchumi kupitia mikopo na uwezeshaji wa makundi maalum.

Ndugu Kawaida anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Mtwara ambapo leo yupo Wilaya ya Tandahimba kwa ajili ya kuzungumza na vijana pamoja na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.

#KaziNaTutuNasongaMbele

#FutureBilaStress

#NeverAgain