Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
RAIS DKT. MWINYI: SERIKALI ZOTE MBILI KUENDELEA KUIMARISHA MUUNGANO. | UVCCM
Habari za Kitaifa (UVCCM) Kipaumbele

RAIS DKT. MWINYI: SERIKALI ZOTE MBILI KUENDELEA KUIMARISHA MUUNGANO.

26 Apr, 2026 Admin User 29 views min read

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar, Dkt.Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali zote mbili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) zitaendelea kuweka mkazo katika kushughulikia changamoto za Muungano ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi, kupitia mifumo ya majadiliano na vikao vya pamoja.

Akizungumza katika kongamano la kuadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Dkt. Mwinyi alieleza kuwa Muungano umeendelea kuwa chombo muhimu cha kuleta mafanikio ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, akiwataka Watanzania kuuenzi, kuulinda na kuudumisha kama urithi wa kihistoria na msingi wa utaifa.

Aidha, aliwahimiza vijana kuwa walinzi wa amani na utulivu wa nchi kwa kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani, huku wakitumia kikamilifu fursa zilizopo katika maeneo ya ajira, elimu na uongozi. Alibainisha kuwa Serikali zimeweka mikakati madhubuti pamoja na rasilimali za kutosha ili kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kitaifa, akieleza kuwa umoja huo ndio nguzo kuu ya kudumisha Muungano, amani na utulivu wa Tanzania. Aliwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha mshikamano huo kwa vitendo na kwa maadili ya uzalendo.