UVCCM yazindua “Kijani Ilani ChatBot
Dar es Salaam – Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohammed Kawaida, ameongoza hafla ya uzinduzi wa Kijani Ilani Chat Bot, programu mpya ya kidijitali inayolenga kuongeza hamasa za kisiasa miongoni mwa vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kawaida alisema kuwa kuimarishwa kwa kampeni za kidijitali ni hatua muhimu ya kuhakikisha vijana wanajitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura.
“Teknolojia hii mpya itakuwa nyenzo muhimu kwa vijana kupata taarifa sahihi za Ilani ya Chama, kujua vipaumbele na sera zetu, na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi,†alisema Kawaida.
Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa UVCCM Taifa, Khalid Mwinyi, alisisitiza umuhimu wa chat bot hiyo katika kuongeza uelewa wa vijana kuhusu dira na sera za chama.
“Tunakaribia uchaguzi mkuu, hivyo kampeni za kidijitali ni nyenzo isiyoepukika. Kupitia Kijani Ilani Chat Bot, vijana watapata fursa ya kujifunza na kuelewa zaidi dira ya chama chetu kuelekea uchaguzi,†alisema Mwinyi.
Aidha, Kawaida aliwataka vijana kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgombea mwenza wake Emmanuel Nchimbi, akiwapongeza kwa hatua ya kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo.
Katika hotuba yake, alitoa pongezi kwa Katibu Mkuu mpya wa UVCCM Taifa, akimweleza kuwa ameandika historia ya kuwa kiongozi mdogo zaidi kushika wadhifa huo na kumhimiza kuhakikisha vijana wanatumia kikamilifu programu mpya ya Ilani ya Chama.
Akihitimisha hotuba yake, Kawaida alisisitiza vijana kupuuza upotoshaji wa mitandaoni unaohusiana na maandamano na badala yake wajikite katika maandalizi ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba.
“Ni wajibu wa kila kijana kuhakikisha anajitokeza kupiga kura. Tuwape mkono Rais wetu na chama chetu kwa vitendo,†alisisitiza.
Mwisho, aliwashukuru vijana wote waliohudhuria hafla hiyo kwa mshikamano wao na mwamko wa kuunga mkono jitihada za chama kupitia nyanja za kidijitali. bofya hapa kutembelea https://kijanichatbot.or.tz/
Habari Zinazohusiana
UVCCM WILAYA YA KAKONKO WAFANYA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA KUZALIWA KWA CCM
01 Feb, 2026
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kakonko umefanya maadhimisho ya kipekee kuelekea miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM, yatakayofanyika rasmi tarehe 5 Februari 2026. Maadhimisho haya yamejumuisha shughuli mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuunga mkono maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
ABUYA AWEKA MSISITIZO KWA VIJANA WA CCM KUKITETEA CHAMA NA VIONGOZI WAKE
31 Jan, 2026
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kigoma, Ndugu Emanuel Abuya, amewataka vijana wa CCM kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutetea, kulinda na kudumisha misingi, sera na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, akisisitiza kuwa hilo ni jukumu la msingi na la kihistoria kwa jumuiya ya vijana.
UVCCM Ngome waadhimisha Kuzaliwa CCM kwa Vitendo, wasafisha Soko la Ngome Iringa
31 Jan, 2026
Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Tawi la Ngome, Kata ya Kihesa, Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa, wamefanya shughuli ya usafi wa mazingira katika Soko la Ngome kama sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).