Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
JESSICA MSHAMA AWANIA NAFASI YA EALA, AAHIDI KUSUKUMA AJENDA YA VIJANA NA TEKNOLOJIA | UVCCM
Habari za Kitaifa (UVCCM) Kipaumbele

JESSICA MSHAMA AWANIA NAFASI YA EALA, AAHIDI KUSUKUMA AJENDA YA VIJANA NA TEKNOLOJIA

22 Apr, 2026 Admin User 66 views min read

Jessica Mshama, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifa, ameendelea kuonesha mwelekeo mzuri wa uongozi na kujiamini mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika tukio lililofanyika Ofisi Ndogo za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam tarehe 20 Aprili 2026.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha hatua hiyo, Mshama alieleza kuwa uamuzi wake wa kuwania nafasi hiyo unatokana na dhamira ya dhati ya kuhakikisha kuwa sauti za vijana, wanawake na makundi yote ya jamii zinapata uwakilishi stahiki katika ngazi ya kikanda. Alisisitiza kuwa Afrika Mashariki ina rasilimali watu yenye nguvu kubwa, lakini bado kuna pengo la ushiriki na upatikanaji wa fursa kwa baadhi ya makundi, jambo ambalo linahitaji uongozi unaoweza kuunganisha sera na mahitaji halisi ya wananchi.

Aliongeza kuwa iwapo atapata nafasi hiyo, atajielekeza katika kusimamia maslahi ya Tanzania kwa weledi na uthabiti, huku akihamasisha ajenda za maendeleo jumuishi zinazolenga kukuza ajira, ujasiriamali, na matumizi ya teknolojia kwa vijana na wanawake. Aidha, alibainisha kuwa atahakikisha uwepo wa sera na maamuzi yanayozingatia usawa kwa makundi yote, ikiwemo yale yaliyo pembezoni, ili kuhakikisha maendeleo ya kikanda yanakuwa ya haki na yanayogusa maisha ya watu kwa vitendo.

Hatua hiyo imepokelewa kwa mwitikio mkubwa kutoka kwa vijana ndani na nje ya UVCCM, ambapo wengi wao wameeleza imani yao kwa uwezo wake wa kuiwakilisha Tanzania katika chombo hicho cha kikanda. Kupitia majukwaa mbalimbali ya kijamii na kisiasa, vijana wameendelea kumpongeza kwa uamuzi huo, wakimtaja kama kiongozi mwenye maono, uthubutu na uelewa wa changamoto halisi zinazowakabili vijana katika zama za uchumi wa kidijitali.
Baadhi ya maoni ya vijana yameeleza kuwa uzoefu wake katika uongozi wa vijana na ushiriki wake katika majukwaa ya kimataifa unampa nafasi ya kipekee ya kusukuma mbele ajenda za kizazi kipya katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wengine wamebainisha kuwa anawakilisha taswira ya uongozi mpya unaojikita katika ujumuishi, ubunifu na matokeo.
Kwa ujumla, vijana wengi wamemtakia kila la heri katika mchakato huo, wakionesha matarajio kuwa anaweza kuwa daraja la kuunganisha ndoto za vijana wa Tanzania na fursa za kikanda ndani ya Afrika Mashariki. Mwitikio wake unaakisi kuongezeka kwa hamasa ya vijana kushiriki kikamilifu katika siasa na uchumi wa kikanda, sambamba na matarajio ya kuona uwakilishi wenye tija katika ngazi ya kikanda.Jessica amekuwa mara nyingi akiwahamasisha vijana