Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
RUNGWA SEKONDARI WAMPONGEZA DKT. SAMIA KWA UJENZI WA MABWENI, MADARASA NA BWALO LA CHAKULA | UVCCM
Habari za Kitaifa (UVCCM)

RUNGWA SEKONDARI WAMPONGEZA DKT. SAMIA KWA UJENZI WA MABWENI, MADARASA NA BWALO LA CHAKULA

19 Apr, 2026 Admin User 41 views min read

Mpanda– Katavi April 18 ,2026

Katibu Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu UVCCM Ndg. Mabula Marco Mabula ametembelea Shule ya Sekondari ya Rungwa yenye wanafunzi kidato cha tano na sita, ambapo alikutana na walimu na wanafunzi waliompongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo shuleni hapo.

Wanafunzi na walimu walieleza kuwa chini ya uongozi wa Dkt. Samia, shule hiyo imenufaika na ujenzi wa mabweni matano mapya, bwalo la chakula, madarasa na maabala ya kisasa ya kujifunzia kwa Wanafunzi wa masomo ya mchepuo wa Sayansi pamoja na kuongezewa bajeti ya uendeshaji wa shule. Walisema miradi hiyo imeongeza ari ya kujifunza na kuboresha hali ya utoaji elimu kwa wanafunzi kuanzia kidato Cha kwanza hadi Cha sita.

Akizungumza na Wanafunzi hao ndg. Mabula Marco Mabula ambaye pia ni Alumni wa shule hiyo 2019-2021, ameeleza kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan:-

1. Elimu bila malipo imepanuliwa kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita, ada ikilipwa na Serikali huku serikali ikiboresha mitaala ya elimu nchini kuendana na mazingira ya Dunia ya Leo.

2. Bajeti ya mikopo ya Elimu ya juu imeongezeka katika kipindi cha miaka mitano (kuanzia 2021/2022 hadi 2025/2026), Serikali imefanikiwa kutoa TZS 3.6 trilioni kwa wanafunzi wa vyuo ngazi ya elimu ya kati na ya juu, hatua iliyowezesha vijana wengi kupata elimu bila vikwazo vya kifedha.

3. Samia Scholarship imenufaisha zaidi ya wanafunzi 2,800 nchini huku Mikopo ya vyuo vya kati yenye thamani ya Bilioni 48 imenufaisha zaidi ya wanafunzi 8,000.

Ndg. Mabula Marco Mabula amewasihi Wanafunzi wa Kidato Cha sita kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu masomo yao ya kidato Cha sita ambapo mitihani itaanza mapema mwezi Mei 2026, na hatimae wafaulu na kupata sifa za kujiuga na masomo ya Elimu ya Juu kupitia Vyuo Vikuu mbalimbali ndani na Nje ya nchi.

Aidha, amewasihi Wanafunzi wa Kidato cha sita watakaochaguliwa kushiriki Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria yenye lengo la kumuandaa kijana awe mkakamavu, mzalendo, mwenye nidhamu, na anayejitegemea katika kulijenga Taifa.

Amehitimisha kwa kuushukuru
Uongozi wa Shule chini ya Mkuu wa Shule ndg. Emmanuel C. Mwamwezi kwa kuendelea kuwa kinara katika kusimamia na kuleta matokeo chanya katika shule hiyo.