Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
MWENYEKITI UVCCM TAIFA ASHIRIKI KUAGA MWILI WA HAYATI LUKUVI | UVCCM
MWENYEKITI UVCCM TAIFA ASHIRIKI KUAGA MWILI WA HAYATI LUKUVI | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari za Kitaifa (UVCCM) Habari ya Kipaumbele

MWENYEKITI UVCCM TAIFA ASHIRIKI KUAGA MWILI WA HAYATI LUKUVI

28 Mar, 2026 00:00 Admin User 22 views 0 comments
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC), ameshiriki katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Isimani na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi.
Ibada hiyo imefanyika leo tarehe 28 Machi 2026 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam, ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hayati Lukuvi alifariki dunia tarehe 25 Machi 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma, akiacha historia ya utumishi uliotukuka kwa taifa katika nyadhifa mbalimbali za uongozi.
Ushiriki wa viongozi mbalimbali, akiwemo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, unaakisi heshima na kuthamini mchango mkubwa wa marehemu katika maendeleo ya nchi.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.