Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
MUENDELEZO WA ZIARA YA KIUTENDAJI KATIKA KATA SITA WAIMARISHA UHAI WA UVCCM | UVCCM
MUENDELEZO WA ZIARA YA KIUTENDAJI KATIKA KATA SITA WAIMARISHA UHAI WA UVCCM | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari za Wilaya

MUENDELEZO WA ZIARA YA KIUTENDAJI KATIKA KATA SITA WAIMARISHA UHAI WA UVCCM

27 Mar, 2026 00:00 Admin User 12 views 0 comments
Katika mwendelezo wa ziara ya kiutendaji katika kata sita, nimekutana na vijana kwa lengo la kuimarisha uhai wa Jumuiya, kuhamasisha usajili wa wanachama wapya na kugawa kadi za uanachama, huku nikisisitiza umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa kadi nyingi kuendelea kusajili vijana kwa wingi.
Aidha, nimepata fursa ya kusikiliza changamoto zinazowakabili vijana na kutoa hamasa ya ushiriki wao katika shughuli za maendeleo pamoja na ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi. Sambamba na hilo, nimesisitiza umuhimu wa kuanzisha miradi ya kiuchumi katika ngazi za matawi na kata ili kuimarisha uwezo wa kifedha wa Jumuiya.
Vilevile, nimehamasisha uundwaji wa vikundi vya vijana kwa ajili ya kunufaika na mikopo ya maendeleo ya jamii, ikiwemo asilimia nne kwa vijana, pamoja na mikopo ya taasisi za kifedha kwa mtu mmoja mmoja. Nimeelekeza umuhimu wa kukopa na kurejesha kwa wakati ili kuongeza uaminifu na kuwezesha wengine kupata fursa kama hizo.
Kwa upande mwingine, nimehimiza mshikamano, upendo, ushirikiano, uwajibikaji na nidhamu miongoni mwa wanachama, pamoja na kujituma katika kazi na kuzingatia maadili ya chama ili kufanikisha maendeleo endelevu ya jamii.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.