Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
ZIARA YA KIUTENDAJI UVCCM (W) TANGA YAANZA KWA KASI KATA YA KIOMONI | UVCCM
ZIARA YA KIUTENDAJI UVCCM (W) TANGA YAANZA KWA KASI KATA YA KIOMONI | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

ZIARA YA KIUTENDAJI UVCCM (W) TANGA YAANZA KWA KASI KATA YA KIOMONI

26 Mar, 2026 00:00 Admin User 20 views 0 comments
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Tanga, Ndugu Salum Dede, leo tarehe 26/03/2026 ameanza rasmi ziara ya kiutendaji katika Kata ya Kiomoni, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhai wa Jumuiya katika ngazi zote.
Katika ziara hiyo, Katibu Dede amekutana na viongozi na wanachama kuanzia ngazi ya kata hadi matawi, akifanya ukaguzi wa uhai wa Jumuiya pamoja na kujadili namna ya kuboresha utendaji wa UVCCM katika maeneo husika.
Aidha, vijana wamepata fursa ya kuwasilisha changamoto mbalimbali, hususan zinazohusu uongozi na maendeleo, ambapo majibu na mwelekeo wa utatuzi umetolewa ili kuhakikisha Jumuiya inaendelea kuwa imara na yenye tija.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.