Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
UVCCM BABATI VIJIJINI YAENDELEA NA ZIARA KATA YA AYASANDA | UVCCM
UVCCM BABATI VIJIJINI YAENDELEA NA ZIARA KATA YA AYASANDA | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari za Wilaya

UVCCM BABATI VIJIJINI YAENDELEA NA ZIARA KATA YA AYASANDA

26 Mar, 2026 00:00 Admin User 17 views 0 comments

Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Babati Vijijini, chini ya Katibu wa Vijana Ndugu George Sanka, imeendelea na ziara ya kiutendaji katika Kata ya Ayasanda leo tarehe 25/03/2026, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhai wa Jumuiya na kuhamasisha ushiriki wa vijana.
Ziara hiyo imelenga kuimarisha Jumuiya, kuhamasisha ulipaji wa ada za uanachama, pamoja na kuwajengea vijana uelewa kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo mikopo inayotolewa kupitia Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Vijana, Wanawake na Wajasiriamali.
Aidha, viongozi wamewahimiza vijana kutembelea na kujifunza kutoka katika miradi mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kuendelea kuitambua na kuisemea vyema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kuleta maendeleo ya wananchi.
Kulinda na Kujenga Ujamaa
Kazi na Utu Tunasonga Mbele
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.