Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
MKALIPA ‘ATIKISA’ KWA OPERESHENI SAMIA KATA ZA MKALAMO NA MKWAJA | UVCCM
MKALIPA ‘ATIKISA’ KWA OPERESHENI SAMIA KATA ZA MKALAMO NA MKWAJA | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

MKALIPA ‘ATIKISA’ KWA OPERESHENI SAMIA KATA ZA MKALAMO NA MKWAJA

25 Mar, 2026 00:00 Admin User 92 views 0 comments
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Pangani, Ndugu Nasri Mkalipa, ameanza rasmi ziara ya siku tisa ya kiutendaji katika kata 14 za wilaya hiyo, akilenga kukutana na makundi mbalimbali ya vijana na kuimarisha uhai wa Jumuiya.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo iliyofanyika Jumanne, Machi 24, 2026, Katibu Mkalipa amekutana na vijana wa Kata za Mkalamo na Mkwaja, ambapo amepata fursa ya kusikiliza changamoto zao na kujadili suluhisho la masuala mbalimbali yanayowakabili. Miongoni mwa keIro zilizojadiliwa ni upatikanaji wa mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri, pamoja na masuala ya maendeleo ya vijana.
Aidha, ziara hiyo imejikita pia katika kukagua uhai wa Jumuiya na kuhamasisha shughuli za michezo, ikiwemo maandalizi ya kuanzishwa kwa mashindano ya mpira wa miguu yanayojulikana kama AWESO Vijana Cup, yenye lengo la kuibua vipaji na kuimarisha mshikamano miongoni mwa vijana.
Ziara hiyo itaendelea kesho Jumatano, Machi 25, 2026, ambapo Katibu Mkalipa anatarajiwa kutembelea Kata ya Kipumbwi kuanzia saa 3:00 asubuhi na baadaye Kata ya Mikinguni saa 8:00 mchana, ikiwa ni mwendelezo wa operesheni hiyo yenye lengo la kuleta mageuzi chanya kwa vijana wa Wilaya ya Pangani.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.