Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
ZIARA YA KATIBU UVCCM WILAYA YA IKUNGI YALETA MAFANIKIO MAKUBWA KATA ZA MKIWA NA ISUNA | UVCCM
ZIARA YA KATIBU UVCCM WILAYA YA IKUNGI YALETA MAFANIKIO MAKUBWA KATA ZA MKIWA NA ISUNA | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

ZIARA YA KATIBU UVCCM WILAYA YA IKUNGI YALETA MAFANIKIO MAKUBWA KATA ZA MKIWA NA ISUNA

25 Mar, 2026 00:00 Admin User 12 views 0 comments
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Ikungi, Ndugu Shabani Iddi Mhimbani, leo Machi 24, 2026 amefanya ziara ya kiutendaji katika Kata za Mkiwa na Isuna, ambapo amekutana na vijana wa kata hizo kwa nyakati tofauti katika ziara iliyozaa mafanikio makubwa.
Katika ziara hiyo, Katibu Mhimbani aliambatana na maafisa wa Benki ya NMB Tawi la Ikungi, ambao walitoa semina fupi kuhusu mikopo ya “Mama Samia” inayolenga kuwawezesha wajasiriamali wadogo. Wameeleza kuwa mikopo hiyo inapatikana kwa masharti nafuu kupitia benki hiyo, ikianzia shilingi 100,000 hadi 4,000,000, huku sharti kuu likiwa ni mhusika kuwa na namba ya utambulisho wa mjasiriamali inayotolewa na halmashauri kupitia maafisa wa maendeleo ya jamii.
Sambamba na hilo, Katibu Mhimbani alisisitiza masuala mbalimbali muhimu ikiwemo uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi ya Jumuiya kwa lengo la kuimarisha uwezo wa kifedha, usajili wa wanachama kupitia mfumo wa kielektroniki, uhamasishaji wa wanachama wapya, pamoja na ulipaji wa ada. Aidha, alikumbusha umuhimu wa kuendesha vikao kwa mujibu wa kalenda ya mwaka 2026 ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi wa uongozi.
Katika hotuba yake, aliwahimiza vijana kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kutumia kikamilifu fursa zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akihitimisha ziara hiyo, Katibu Mhimbani aliwasihi vijana kuwa wazalendo, akisisitiza kuwa vijana ni nguvu kazi ya taifa na tegemeo muhimu la Chama Cha Mapinduzi katika kujenga maendeleo endelevu.
Taarifa hii imetolewa na Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Ikungi
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.