Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
ZIARA YA KITENDAJI YANZA KATA ZA MABWEPANDE NA BUNJU | UVCCM
ZIARA YA KITENDAJI YANZA KATA ZA MABWEPANDE NA BUNJU | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

ZIARA YA KITENDAJI YANZA KATA ZA MABWEPANDE NA BUNJU

25 Mar, 2026 00:00 Admin User 18 views 0 comments
Tarehe 24 Machi, 2026, nimeanza ziara ya kikazi katika Kata za Mabwepande na Bunju kwa lengo la kukagua uhai wa Jumuiya, kufuatilia shughuli za UVCCM pamoja na kuzungumza na viongozi na wanachama katika ngazi mbalimbali.
Katika ziara hiyo, nimewapongeza wanachama wa UVCCM katika kata hizo kwa ushiriki wao mzuri katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, uliosaidia kupatikana kwa ushindi wa kishindo kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa CCM pamoja na Madiwani wa CCM. Aidha, nimewasisitiza kuendelea kuwa mabalozi wa amani, umoja na maendeleo ya Taifa letu.
Vilevile, nimewakumbusha viongozi wa kata na matawi umuhimu wa kuzingatia nidhamu ya uongozi, kufuata kanuni za Jumuiya, na kufanya vikao vya kikanuni kwa wakati ili kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha Jumuiya na kujenga uongozi imara na wenye tija.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.