Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KATIBU UVCCM (W) SONGEA MJINI AFANYA ZIARA YA KITENDAJI KATA MBILI | UVCCM
KATIBU UVCCM (W) SONGEA MJINI AFANYA ZIARA YA KITENDAJI KATA MBILI | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

KATIBU UVCCM (W) SONGEA MJINI AFANYA ZIARA YA KITENDAJI KATA MBILI

24 Mar, 2026 00:00 Admin User 29 views 0 comments
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Songea Mjini, Ndugu David J. Mlonga, ameendelea na ziara ya kitendaji katika Kata mbili, M/Mshindo na Mjimwema, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhai wa Jumuiya na kuhamasisha ushiriki wa vijana.
Katika ziara hiyo, ambayo inalenga kukagua shughuli za Jumuiya na kuhamasisha mshikamano, Katibu Mlonga aliwaeleza vijana umuhimu wa kuitumikia Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM kwa nguvu zote, kwa uzalendo mkubwa, na kujitahidi kuanzisha miradi mipya ya kiuchumi katika ngazi zote za kata na matawi.
Katibu Mlonga alisisitiza kuwa kuanzisha miradi ya kiuchumi kutaleta nguvu ya kifedha ndani ya Jumuiya na kuhakikisha shughuli zake zinaendeshwa kwa urahisi bila vikwazo, hali inayohakikisha Jumuiya inaendelea kuimarika na kutoa fursa za maendeleo kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.