Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
ZIARA YA KATIBU UVCCM IRINGA MJINI YAIMARISHA MSHIKAMANO KATA YA ISAKALILO | UVCCM
ZIARA YA KATIBU UVCCM IRINGA MJINI YAIMARISHA MSHIKAMANO KATA YA ISAKALILO | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

ZIARA YA KATIBU UVCCM IRINGA MJINI YAIMARISHA MSHIKAMANO KATA YA ISAKALILO

24 Mar, 2026 00:00 Admin User 23 views 0 comments
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Iringa Mjini, Ndugu Bagaya, leo Machi 23, 2026, amefanya ziara ya kiutendaji katika Kata ya Isakalilo, akikutana na vijana wa eneo hilo kwa lengo la kuimarisha mshikamano, ushirikiano na uwajibikaji ndani ya Jumuiya.
Ziara hiyo imelenga kuhuisha uhai wa UVCCM kuanzia ngazi ya matawi, kata hadi wilaya, ambapo Katibu Bagaya alisisitiza umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za Jumuiya pamoja na maendeleo ya jamii.
Katika mazungumzo yake, amewahimiza vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ya CCM, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri (4:4:2) pamoja na mikopo ya wajasiriamali binafsi inayotolewa na taasisi za kifedha kama NMB Bank. Amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutumia fursa hizo ili kujikwamua kiuchumi.
Aidha, Katibu Bagaya alibainisha kuwa siasa na uchumi vina uhusiano wa karibu, hivyo ni wajibu wa vijana kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali ili kuleta maendeleo yao binafsi na ya jamii kwa ujumla.
Ziara hiyo imeambatana na uwepo wa viongozi mbalimbali wa wilaya, hali inayoonesha mshikamano wa uongozi katika kusukuma mbele ajenda za vijana.
Kazi na Utu Tunasonga Mbele 🔰🔰
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.