Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KATIBU UVCCM WILAYA YA KONDOA AFANYA ZIARA KATIKA KATA TATU KUIMARISHA JUMLA YA SHUGHULI ZA VIJANA | UVCCM
KATIBU UVCCM WILAYA YA KONDOA AFANYA ZIARA KATIKA KATA TATU KUIMARISHA JUMLA YA SHUGHULI ZA VIJANA | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

KATIBU UVCCM WILAYA YA KONDOA AFANYA ZIARA KATIKA KATA TATU KUIMARISHA JUMLA YA SHUGHULI ZA VIJANA

24 Mar, 2026 00:00 Admin User 24 views 0 comments
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Kondoa ameendelea na ziara ya kitendaji katika kata za Bolisa, Kondoa Mjini na Kilimani, kwa lengo la kuimarisha uhai wa Jumuiya na kusikiliza changamoto zinazowakabili vijana katika maeneo hayo.
Katika ziara hiyo, Katibu amekutana na Mabaraza ya Vijana ya Kata, ambapo amepata fursa ya kufanya tathmini ya uhai wa Jumuiya, kupokea kero mbalimbali za vijana pamoja na kujadili njia mbadala za kuzitatua kwa ufanisi. Aidha, masuala mengine yanayohusu maendeleo ya vijana na uendeshaji wa Jumuiya yamejadiliwa kwa kina ili kuongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.
Ziara hiyo imefanyika kwa ushirikiano na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Wilaya ya Kondoa, ambao wameambatana na Katibu katika kuhakikisha malengo ya ziara yanafikiwa na kuleta matokeo chanya kwa vijana na Jumuiya kwa ujumla.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.