Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KATIBU UVCCM (W) MBARALI AENDELEA NA ZIARA YA KITENDAJI KATA YA UBARUKU | UVCCM
KATIBU UVCCM (W) MBARALI AENDELEA NA ZIARA YA KITENDAJI KATA YA UBARUKU | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

KATIBU UVCCM (W) MBARALI AENDELEA NA ZIARA YA KITENDAJI KATA YA UBARUKU

23 Mar, 2026 00:00 Admin User 28 views 0 comments
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Mbarali, Cde. Juma Shabani Hatibu, ameendelea na ziara ya kitendaji katika kata mbalimbali, ambapo leo tarehe 23/03/2026 ametembelea Kata ya Ubaruku kwa lengo la kuimarisha shughuli za Jumuiya na kusikiliza changamoto za vijana.
Katika ziara hiyo, Cde. Hatibu alikutana na vijana wa matawi pamoja na viongozi wa ngazi ya kata wa UVCCM, ambapo alipata fursa ya kusikiliza kero zao, kupokea maoni na ushauri, pamoja na kushughulikia baadhi ya changamoto zilizowasilishwa. Ziara hiyo pia imekuwa chachu ya kuhuisha na kuamsha ari ya ushiriki wa vijana ndani ya Jumuiya.
Aidha, Katibu aliwahamasisha vijana kujikita katika kutafuta na kutumia fursa za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi ya maendeleo itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi. Vilevile, aliwahimiza kulipa ada za uanachama kwa wakati ili kuimarisha uhai na uendeshaji wa Jumuiya.
Akihitimisha ziara hiyo, Cde. Hatibu aliwasisitiza vijana kudumisha uzalendo, kuipenda nchi yao, na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.