Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
RAIS DKT. MWINYI AFUTURISHA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI PEMBA | UVCCM
RAIS DKT. MWINYI AFUTURISHA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI PEMBA | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

RAIS DKT. MWINYI AFUTURISHA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI PEMBA

11 Mar, 2026 00:00 Admin User 25 views 0 comments
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika futari ya pamoja aliyowaandalia.
Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 11 Machi 2026 katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi, Mkoa wa Kusini Pemba, ambapo pia imehudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi.
Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa utaratibu wa kufutari pamoja unaleta upendo, mshikamano na umoja miongoni mwa wananchi, na kuwashukuru wote walioshiriki katika futari hiyo.

Futari hiyo imewajumuisha watu wa makundi mbalimbali wakiwemo mayatima, wajane, watu wenye ulemavu, walimu wa madrasa, masheikh na maimamu wa Mkoa wa Kusini Pemba.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Shehe Hassan Shaaban amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa matendo mema, fadhila na wema anaowaonesha wananchi, ikiwemo kuwaandalia futari hiyo, na kumtakia uongozi mwema na mafanikio.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.