Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
DKT. SAMIA SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA WANAWAKE TANZANIA | UVCCM
DKT. SAMIA SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA WANAWAKE TANZANIA | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

DKT. SAMIA SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA WANAWAKE TANZANIA

08 Mar, 2026 00:00 Admin User 62 views 0 comments
Na Mwandishi Wetu, Emmanuel Peter Frednand
Tarehe 8 Machi ya kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa lengo la kutambua mchango mkubwa na muhimu wa wanawake katika maendeleo ya jamii tunazoishi. Maadhimisho haya pia hutumika kutathmini hatua zilizopigwa katika kukuza usawa wa kijinsia na kuimarisha nafasi ya mwanamke katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha juhudi, nguvu na mchango wa mwanamke vinatambuliwa na kupewa nafasi stahiki katika kulisukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa la Tanzania. Kupitia sera, mipango na maamuzi ya kimkakati ya serikali yake, wanawake wameendelea kunufaika na fursa mbalimbali

  katika elimu, uchumi, afya na ustawi wa kijamii.
Kupitia Maendeleo ya Elimu kwa Wanawake
Rais Dkt. Samia amefanikisha ujenzi wa shule 26 za sekondari za sayansi kwa wasichana nchini. Hatua hii imelenga kuongeza ushiriki wa wasichana katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM). Tayari wanafunzi zaidi ya 48,000 wameanza kusoma katika shule hizo, jambo linaloimarisha msingi wa kizazi kipya cha wanawake wataalamu katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Katika Nyanja ya Uchumi
Dkt. Samia hajawaacha nyuma wanawake katika safari ya maendeleo ya kiuchumi. Serikali yake imeendelea kuimarisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kupitia halmashauri za nchi nzima, ambapo wanawake ni miongoni mwa walengwa wakuu wa mpango huo.
Aidha, kupitia ushirikiano kati ya serikali na taasisi za kifedha kama CRDB Bank na NMB Bank, wanawake wajasiriamali wamepata fursa ya mikopo ya kibenki kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara zao (start-ups). Katika mfumo huo wa mikopo, wanawake wamepewa kipaumbele ili kuongeza uwezo wao wa kiuchumi na kupanua shughuli za uzalishaji na biashara.
Pia, Rais Dkt. Samia ameelekeza utolewaji wa elimu ya ujasiriamali katika ngazi za halmashauri na mikoa kupitia wizara husika, ambapo kundi la wanawake limepewa kipaumbele kikubwa katika kushiriki mafunzo hayo ili kuongeza ujuzi wa biashara, usimamizi wa fedha na ubunifu wa kiuchumi.
Mbali na hilo, Dkt. Samia ametoa kipaumbele kwa wanawake kupata fursa za zabuni za serikali. Kupitia sera za manunuzi ya umma, wanawake wajasiriamali wamepewa nafasi maalum katika baadhi ya zabuni za serikali, hatua inayochochea ukuaji wa biashara zao na kuongeza ushiriki wao katika uchumi wa taifa.

Katika Sekta ya Afya kwa Wanawake
Katika kuimarisha huduma za afya kwa wanawake, Dkt. Samia amesimamia ujenzi wa hospitali mpya zaidi ya 400 pamoja na vituo vipya vya afya zaidi ya 956 nchini. Miundombinu hii imeongeza upatikanaji wa huduma za afya ya mama na mtoto katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Hatua hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua. Awali kiwango cha vifo vya akina mama kilikuwa vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000. Hata hivyo, kutokana na uboreshaji wa huduma za afya ya mama na mtoto, kiwango hicho kimepungua hadi kufikia takribani vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000.
Katika Kuinua Ustawi wa Mwanamke katika Jamii
Katika kupambana na ukatili wa kijinsia, Dkt. Samia amechukua hatua madhubuti za kuimarisha ulinzi na haki za wanawake. Serikali imeongeza uwezo wa madawati ya jinsia katika vituo vya polisi nchini kote ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.
Vilevile, kuanzia ngazi ya vijiji, halmashauri hadi wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, elimu imekuwa ikitolewa kwa jamii kuhusu usawa wa kijinsia, haki za wanawake na umuhimu wa ushiriki wao katika maendeleo ya jamii. Elimu hiyo pia inalenga kupinga na kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Dkt. Samia Amewasaidia Wanawake Kupitia Huduma za Kisheria
Kupitia mpango wa Mama Samia Legal Aid, huduma za msaada wa kisheria zimeboreshwa na kupatikana katika mikoa yote nchini. Mpango huu umewezesha zaidi ya wanawake milioni moja kupata huduma za kisheria bure.
Kupitia huduma hiyo, wanawake wengi wamepata msaada katika utatuzi wa migogoro ya ardhi, mirathi na ndoa. Aidha, Rais Samia aliiagiza Wizara ya Ardhi kutoa msaada pamoja na kuweka wazi mawasiliano ya makamishna wa ardhi katika mikoa yote ili kurahisisha utatuzi wa changamoto za ardhi kwa ufanisi na kwa haraka.
Hivyo basi, ni dhahiri kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuwa kinara katika juhudi za kuimarisha ustawi wa wanawake nchini Tanzania. Kupitia sera, mipango na hatua mbalimbali za maendeleo, wanawake wameendelea kupata nafasi kubwa zaidi katika elimu, uchumi, afya, haki za kisheria na uongozi, jambo ambalo linaimarisha msingi wa maendeleo jumuishi ya taifa.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.