Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
CCM na FRELIMO Kuimarisha Ushirikiano wa Kiuchumi | UVCCM
CCM na FRELIMO Kuimarisha Ushirikiano wa Kiuchumi | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

CCM na FRELIMO Kuimarisha Ushirikiano wa Kiuchumi

06 Mar, 2026 00:00 Admin User 33 views 0 comments
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha‑Rose Migiro, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa FRELIMO wa Msumbiji, Chakil Felizardo Passadas Aboobacar, ambaye ameanza ziara rasmi ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 6 Machi 2026 katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Offices, ambapo viongozi hao wamejadili namna ya kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya vyama hivyo viwili.
Katika mazungumzo yao, CCM na FRELIMO vimekubaliana kuongeza ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo, hususan katika sekta za uchumi, biashara na uwekezaji, kwa lengo la kuimarisha ustawi wa wananchi wa nchi hizo mbili.
Vyama hivyo viwili vina historia ndefu ya ushirikiano wa kisiasa na kiitikadi tangu kipindi cha harakati za ukombozi wa kusini mwa Afrika, ambapo Tanzania ilikuwa kitovu muhimu cha kusaidia harakati za ukombozi za nchi mbalimbali za ukanda huo, ikiwemo Msumbiji.
Ziara ya Katibu Mkuu wa FRELIMO nchini Tanzania inalenga pia kuendeleza mazungumzo ya kimkakati kati ya vyama hivyo kuhusu masuala ya maendeleo, utawala bora, na kuimarisha mahusiano ya kihistoria yaliyodumu kwa miongo kadhaa.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.